ダルエスサラーム便り


Habari za Dar es Salaamタンザニアからの手紙Kusikia si kuona
Pole PoleHabari kutoka Lukani歴代スタッフのHabariの本棚


キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira

Yaummy Nyombe ヤウミ

Habari kutoka Kingolwira -No.17



Mnamo tarehe 03 June 2014 kwa mara ya kwanza kijiji cha Kingolwira kimepokea mgeni kutoka nchini Sudan ya Kusini Mr. Ayo Peter Wani.

Alifika na kuweza kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo shamba kubwa mojawapo la kilimo cha mkonge linalimilikiwa na wazawa kwa maana ya Watanzania kwa kipindi hiki na kukutana na Meneja wa shamba hilo anyeitwa Mr. Bahati BASIL na kuweza kufanya nae mazungumzo ya ana kwa ana kwa takribani muda wa masaa mawili, aliweza kumpa historia ya mkonge kwa nchini Tanzania kwa ujumla pia kumueleza mwaka ambao shamba lile limeanzishwa na jinsi uzalishaji wake ulivyo wakati huo mpaka kufikia sasa hivi na changamoto nyingi walizonazo katika uzalishaji, baada ya kumaliza tukaingia ndani ya kiwanda na kujionea mashine ya kusaga mkonge na kutoa singa kwa jina lake maarufu (Corona), baada ya hapo ziara ileikawa imeishia pale.

Pia tuliweza kufika katika shamba la Miti kwa lugha ya Kiswahili inaitwa Mibono na lugha ya kiitaalam ni JATROPHA, shamba hilo lina ukubwa wa Ekari hamsini na liko umbali wa kama kilomita tano kutoka kijiji cha Kingolwira.Shamba hilo linamilikiwa na kampuni ya kijapan iitwayo SEKISUI lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kupata maelezo makubwa ya shamba hilo kutoka na wamiliki hawakua jirani na pale kijijini ila tulifanikiwa kuongea na simu na bwana Haruna Ngubi ambaye mwanzoni alikua msimamizi wa shamba hilo lakini kwa sasa yuko mkoani Pwani anasimamia shamba lingine aliweza kutupa maelezo kiasi kwa njia ya simu.

Vile vile tulifanikiwa kutembelea katika shamba la mahindi la mkulima wa kawaida ambaye amelima heka mbili kwa njia ya mkono na wakati ule ulikua ni muda ambao mahindi yameanza kukauka na yeye anajiandaa kwa ajili ya kutaka kufanya mavuno, lakini kwa mwaka wa 2014 kilimo hakikuwa vizuri kwa kuwa mvua ilikua kubwa mno na sehemu kubwa ya mashamba mengi mazao yalikua yameharibika, lakini kwa kiasi kikubwa kwa hali ya chakula sio mbaya sana.

Pia tulifika katika mradi wa kuku ambao ni NGO iliyoko kilomita tatu kutoka kijiji cha Kingolwira ila kwa bahati mbaya wahusika wote hawakuweza kuwepo katika factory kwa hiyo hatukufanikiwa kuingia ndani.

Na mwishoni tulitembea kijiji cha wamaasai kilichopo umbali wa kiliomita tano kutoka kjijini Kinglowira na kuweza kuona maisha ya kabila hilo ambalo mpaka sasa hivi wamezeka kudumisha mila zao ikiwepo mavazi yao ambayo huwa ni kama nguo za kujifunika na pia kuishi na mifugo pamoja ikiwamo ng`ombe, mbuzi, punda nk.

Na siku ya mwisho tulipita katika shule ya msingi Kingolwira na bwana Ayo Peter aliweza kutoa mchango wake kiasi cha Shilingi za Tanzania Arobaini elfu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ambao tumekuta ukiendelea na mwalimu mkuu na walimu wa shule ya Kingolwira walimshukuru sana kwa ukarimu wake kutoka nchini Sudani Kusini na kuweza kuchangia ujenzi wa shule katika nchi nyingine.

Baada ya hapo basi siku iliyofuatia tulifanya safari ya kurudi Dar es salaam

(1/07/2014)




 6月3日にキンゴルウィラ村に南スーダンからのお客さん、アヨ・ペーター・ワニさんが来てくれました。

 アヨさんはいろいろな場所を訪問しました。広大な農場にも。その一つはサイザル麻の現在タンザニア人によって所有されている農場でした。農場のマネージャーのバハリ・バシルさんにお会いしました。彼とは、タンザニアにおけるサイザル麻栽培の歴史や、農場を始めてから現在に至るまでの生産量やその生産への今までのたくさんの努力などについて向かい合って約2時間もの間、話をしました。その後、工場内へ入り、コロナという有名な名前を持つサイザル麻を砕いて、紐にしていく機械を見ました。そしてここへの訪問を終えました。

 また、ジャトロファ農場にも行きました(スワヒリ語ではミボノ)。この農場は5エーカーもの広さがあり、キンゴルウィラ村からは5kmほど離れています。ここは日本の会社の積水が所有していますが、あいにく所有者が近くにいなかったので、詳しい説明を得ることができませんでした。この農場の管理人で、現在は海岸地域の別の農場の管理人をしているハルナ・グビさんとは、村から電話で話すことができ、簡単な説明を得ることはできました。

 また、機械を使わずに2エーカーの畑にトウモロコシを植えた村の農民の畑へも行きました。ちょうど収穫のためにトウモロコシを乾かし始めたところでした。しかし、2014年は降雨量が非常に多すぎ、広い地域の多くの畑で、農作物がダメになりました。でも、食料の多くはそれほど悪い状態ではありません。

 村から3km離れた場所で養鶏プロジェクトを行なっているNGOのところへも行きました。でも運悪く、関係者がぜんぜんいなかったので、養鶏場の中に入ることができませんでした。

 最後にわたしたちは、村から5km離れたマサイの村へ行きました。マサイたちが現在に至るまで彼らの伝統が受け継がれています。体を覆うような服装とか牛やヤギやロバなどの家畜と一緒に暮らしていることなどを見ることができました。

 最終日にアヨさんとキンゴルウィラ小学校を訪れました。アヨさんは学校の教室建設のために4万シリングを小学校に寄付してくれました。校長と先生方は南スーダンという外国から来たのに、この国の学校建設に寄付を寄せてくれたアヨさんの親切にたいへん感謝しました。

 その後、ダルエスサラームに戻りました。

(2014年7月1日)


サイザル麻の工場/Kiwanda cha mkonge©Ayo Peter

ジャトロファ農場/Shamba la mibono©Ayo Peter


バックナンバーへ

キンゴルウィラ村へのお誘いへ

トップページへ戻る